Song of the Tanzanian Immigration Force - Wimbo Maalumu wa Jeshi la Uhamiaji Tanzania

Song of the Tanzanian Immigration Force - Wimbo Maalumu wa Jeshi la Uhamiaji Tanzania
 

Mimi ni mlinzi wa milango ya kuingia nchi

Mimi ni afisa uhamiaji,

Najua majukumu niliyonayo,

Kwa Tanzania nchi yangu,

Naapa sitorudi nyuma,

Kwa nidhamu upendo mshikamano

Naahidi nitawajibika na kuikataa rushwa kweli,

Adui wa maendeleo.


Kazi na wajibu ni kudumisha,

Usalama na kuleta maendeleo

Kwa Tanzania nchi yangu,

Naapa sitorudi nyuma,

Uraia kwa mtu stahiki,

Pasi na vibali vya ukazi,

Pasipoti hati za safari nitoe kwa sheria kweli.


Kudumisha usalama mahusiano 

Ya nchi yangu Tanzania mataifa mengine,

Kuwekeza fursa za kiuchumi kwa raia na wageni niwajibike

Kwa nidhamu upendo mshikamano

Naahidi nitawajibika,

Chini ya sheria za uhamiaji pia nazo sheria za nchi.


Damu yangu imejaa Utanzania,

Ardhi yake ninapaswa kuilinda kwa moyo,

Dhidi yao wahamiaji haramu pia wahamiaji kimagendo,

Mimi ndiye mlinzi wa milango,

Kuingia kutoka nchini,

Mungu nakuomba unisaidie,

Tanzania yanitegemea.

Comments

Popular posts from this blog

Katyusha - Катюша (Kazakh Ver.)

The Song of Salt - Солёная песня

Chceme Nazad Košice